2 Samuel 5:17-22

17 aWafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 18 bBasi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 19 ckwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.”

20 dNdipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.
Maana yake Bwana Afurikae.
21 fWafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua.

22Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai.
Copyright information for SwhKC